Kikosi
cha Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa
wasichana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania (Tanzanite)
kinatua nchini Alhamisi (Desemba 5 mwaka huu).
Afrika
Kusini ambayo itafikia hoteli ya Sapphire itatua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana kwa ndege
ya South Africa Airways.
Mechi
hiyo itachezeshwa na refa Nabikko Ssemambo kutoka Uganda wakati mwamuzi
msaidizi namba moja ni Gebreyohanis Trhas kutoka Ethiopia. Waamuzi
wengine ambao pia wanatoka Uganda ni Nakitto Nkumbi na Irene Namubiru.
Kamishna
wa mechi hiyo ni John Muinjo kutoka Namibia. Muinjo pia ni Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Miguu Namibia (NFA) na mjumbe wa Kamati ya Mpira
wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Viingilio
katika mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) kuanzia
saa 10 kamili jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 1,000 kwa viti
vya rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa
VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.
Tanzanite
chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa mechi hiyo. Kambi ya
Tanzanite hivi sasa imehamia Msimbazi Hotel kutoka Ruvu mkoani Pwani.
0 maoni:
Post a Comment