Bingwa mtetesi MANCHESTER UNITED imeendelea
kusuasua baada ya kuchapwa na TOTTENHAM HOTSPUR bao mbili kwa moja katika
uwanja wao wa nyumbani wa OLD TRAFFORD.
Alikuwa mchezaji Nyota wa Togo Emmanuel
Adebayor alianza kuipatia timu yake bao la kuongoza dakika ya 34 ya mchezo
,wakati Manchester united wakiendelea kujiuliza mchezaji CHRISTIAN ERIKSEN
aliongeza bao la pili kwa timu yao mnamo dakika ya 66 kipindi cha pili.
MANCHESTER UNITED walikuja juu dakika ya 68
mchezaji DANNY WELBECK aliifungia timu yake bao la kwanza na kuendelea kuwa na
matumani ya kuweza kusawazisha.
Lakini hadi dakika tisini MANCHESTER UNITED
wakalala kwa bao mbili kwa moja na kushika nafasi ya saba katika msimamo wa
ligi.
Chelsea wao wameendelea kubakia nafasi ya
tatu katika msimamo wa ligi baada ya kuifumua timu ya SOUTHAMPTON mabao matatu
kwa bila katika mchezo uliopigwa uwanja wa ST MARYS.
Mabao ya FERNANDO TORRES na wachezaji
waliotoka benchi, WILLIAN NA OSCAR, yote katika kipindi cha pili, yalikamilisha
ushindi huo wa ugenini kwa vijana wa Jose Mourinho walioendeleza matumaini yao
ya kunyakua taji.
CHELSEA walibakia nafasi ya tatu, alama moja
nyuma ya MANCHESTER CITY na mbili nyuma ya viongozi ARSENAL baada ya kivumbi
hicho kilichoandaliwa uwanja wa St Mary’s.
Kwa mara nyingine tena, nyota LUIS SUAREZ, alikuwa
kigezo cha Liverpool pale alipowaongoza kupanda hadi nafasi nne bora za Ligi ya
ENGLAND kwa kuibuka na ushindi wa mbao mawili kwa bila dhidi ya HULL CITY.
Baada ya kupoteza mechi mbili dhidi ya waasimu wao wa kuwania taji, MANCHESTER
CITY NA CHELSEA, kikosi cha BRENDAN RODGERS kilirejelea tena utawala kupitia
makali ya Suarez.
Mlinda ngome DANIEL AGGER aliwapatia uongozi
kupitia kichwa kwenye kipindi cha kwanza kabla ya Suarez kuwaduwaza mashabiki
wa HULL CITY tena na mkwaju wa adhabu
katika dakika ya 50 na kutinga nyavuni.
ARSENAL walikaribisha mwaka wa 2014 na
ushindi wa 2-0 dhidi ya CARDIFF CITY na kudumisha uongozi wao mwembamba
kileleni mwa Ligi hiyo.
Ingawa waliweza kutamba, Arsenal walionekana
kukosa ubunifu wa kupenya ngome ya CARDIFF
CITY .
ARSENAL ilianza kupata bao la kuongoza
kupitia kwa mchezaji , NICHOLAS BENDTNER, aliyempumzisha, LUKAS PODOLSKI, katika
kipindi cha pili.
THEO WALCOTT alihakikisha ushindani kwa
kuzamisha la pili katika muda wa majeruhi huku ushindi huo ukiongezea tetesi
kwamba huu huenda ukawa musimu ambao kikosi cha ARSENE WENGER, kitafanikiwa
kusitisha ukame wao wa taji la ENGLAND.
Mabao hao ya dakika za mwisho mwisho
yaliwezesha Arsenal kurejea tena kileleni baada ya MANCHESTER CITY kuchukua
uongozi wa muda pale walipokamilisha ushindi wa 3-2 ugenini Swansea.
FERNANDINHO aliwapatia CITY uongozi kabla ya WINFRIED
BONY kusawazisha katika kipindi cha kwanza.
YAYA TOURE NA ALEXANDER KOLAROV waliongezea
wageni mabao ya pili na tatu kipindi cha lala salama kabla ya Bony kupata lake
la pili dakika ya mwisho.
Kwingineko, CRYSTAL PALACE walitoka sare ya
1-1 na NORWICH CITY nao FULHAM walijipatia matumaini ya kuepuka kushuka daraja
kwa kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya
West Ham waliosalia taabani.
STOKE CITY walilazimishwa sare ya 1-1 na
wageni Everton huku akisawazisha na penalti katika muda wa ziada.
ASTON VILLA walisherehekea ushindi nadra wa
1-0 ugenini SUNDERLAND waliobaki wakivuta mkia wa msimamo wa ligi
Newcastle kwa upande wao walifumuliwa bao moja kwa bila
dhidi ya wenyeji West Brom.
0 maoni:
Post a Comment