Thursday, January 9, 2014

MAPINDUZI SIMBA USO KWA USO NA URATimu ya SIMBA imeungana na timu ya AZAM, URA na KCC katika nusu fainali ya michuano ya mapinduzi baada ya kuifunga CHUONI mabao mawili kwa bila katika mchezo uliofanyika usiku uwanja wa AMAN.

Alikuwa mchezaji RAMADHAN SINGANO ndiye aliyeipeleka timu ya SIMBA nusu fainali baada ya kuifungia mabao yote mawili kipindi cha pili.

Mabao ya SINGANO yalifungwa dakika ya 48 na dakika ya 58 ya mchezo.

Nusu fainali ya michuano hiyo itakuwa siku ya IJUMAA ambapo SIMBA itakutana na URA ya UGANDA wakati timu ya AZAM itacheza nusu fainali na KCC nayo ya UGANDA.

AZAM imetinga nusu fainali baada ya kuifunga CLOVE STAR kombani ya PEMBA kwa mabao mawili kwa bila.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU