Saturday, January 25, 2014

UJUMBE WA SERIKALI YA CHINA WIZARA YA HABARI

 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Prof: Hermas Mwansoko akiongea na Ujumbe kutoka Serikali ya China kuhusu Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kichina  na maadhimisho ya Miaka 50 ya Kidiplomasia baina ya China na Tanzania yatakayofanyika katika Uwanja wa Uhuru kesho, mgeni rasmi atakuwa Mhe.Mizengo Pinda Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Prof: Hermas Mwansoko (Kulia) akipokea Kitabu chenye Historia ya Mchezo wa Karate kutoka kwa mmoja wa wachezaji wa Mchezo huo Shi yan Cen (Kushoto) ikiwa ni ishara ya kuendelea kudumisha ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na China.(Picha zote na Benjamin Sawe wa Wizara ya
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Prof: Hermas Mwansoko akisikiliza jambo kutoka kwa Mshauri wa Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Nchini Liu Dong wakati ujumbe huo ulipomtembelea Ofisini kwake juu ya maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kichina  na maadhimisho ya Miaka 50 ya Kidiplomasia baina ya China na Tanzania yatakayofanyika katika Uwanja wa Uhuru kesho

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU