Thursday, January 30, 2014

UNIC yaendelea kutoa mafunzo ya mateso ya kambi za wayahudi

DSC_0014
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond juu ya umuhimu wa kujifunza mauaji ya kimbari ya wayahudi ya mwaka 1933.
Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimeendelea kutoa mafunzo na elimu juu ya umuhimu wa kukumbuka maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya ukombozi wa kambi za mateso ya Auschwitz kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond ya jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Afisa habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba ni muhimu kwa kizazi na kizazi kujifunza madhara ya mauaji na maangamizi ya moto dhidi ya wayahudi yaliofanywa na askari wa kinazi wa Ujerumani.
“Ni muhimu kutoa mafunzo kwa vijana wakitanzania wa shule za msingi na sekondari ili wajue kwamba tofauti za rangi na za kidini hazina nafasi ya kutugawa kama binadamu,” amesema Nkhoma.
DSC_0005
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Diamond na Mlezi wao wakimsikiliza Bi. Ledama (hayupo pichani).
DSC_0044
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiafa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto.
Alisisitiza kwamba mauaji na mateso ya Auschwitz yalipoteza mamilioni ya watu wasio na hatia na mafunzo haya yanaonyesha chuki na ubaguzi dhidi ya wayahudi na chuki za aina nyingine yoyote hazina nafasi katika ulimwengu wa leo.
Nkhoma amesema kwamba binadamu wote ni sawa na tofauti za kipato au dini au rangi haziwezi tena kujenga chuki dhidi ya binadamu wengine kwa sababu wote kama binadamu tuna haki sawa mbele za mungu.
DSC_0051
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond jijini Dar es Salaam, wakifuatilia sinema maalum ya mauaji ya kambi za mateso ya wayahudi mwaka 1933.
Wakati huo huo, ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto amesema aliona makambi ambako wayahudi, waroma, wasinti, mashoga, wafungwa wa kivita na watu wenye ulemavu walitumia siku za mwisho katika hali ya kinyama.
“Umoja wa Mataifa ulianzishwa kuzuia kila aina hii ya fazaa kutokea tena, lakini bado misiba kuanzia Cambodia hadi Rwanda mpaka Srebrenica inaonyesha kuwa sumu ya mauaji ya kimbari bado inatiririka,” ilisema taarifa hiyo.
DSC_0082
Pichani juu na chini ni Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond wakisoma baadhi ya machapisho ya Umoja wa Mataifa.
DSC_0077
DSC_0075

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU