Thursday, February 20, 2014

Mafunzo ya TEHAMA kwa Simu yasisitizwa kukuza Demokrasia Vijijini

IMAG0271
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Kilombero, Hassan Masala, akifungua mafunzo ya matumizi ya simu kwa habari katika ukumbi wa Mazingira Kibaoni, Ifakara 03 Februari 2014 yanayolenga kukuza taaluma ya upashaji habari kwa kutumia simu. Kushoto ni Afisa Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bi. Christa Njovu na Kulia ni Mkufunzi kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu.
Na. Mwandishi wetu
Demokrasia vijijini itapatikana iwapo vyombo vya habari jamii vitatumika kikamilifu na kutekeleza wajibu wake wa kupasha habari kwa kutumia teknolojia mpya.
Akifungua mafunzo ya wiki moja katika Ukumbi wa Mazingira, Kibaoni Ifakara yanayowashirikisha wanahabari jamii kutoka Pemba, Unguja, Pangani, Ifakara na Kyela, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Hassan Masala amesema mbinu za kisasa zinahitajika kuelimisha jamii na mambo gani yafanyike ili kupata uongozi bora vijijini na taifa kwa ujumla.
20140204_111348
Mkufunzi wa Teknolojia ya simu kwa habari kutoka Chuo Kikuu Bibi Faith Shayo akifafanua jinsi simu za “SMART” zinavyoweza kutumika kwa habari mbalimbali, picha na maoni kutoka na kwenda katika jamii kupitia maelekezo husika yaliyomo katika simu.
Bwana Masala amesema pamoja na changamoto zilizoko vijijini, Redio Jamii Pambazuko iliyoko Ifakara, ina mchango mkubwa katika kuelimisha na kukuza demokrasia katika wilaya ya Kilombero kwa kuwa inafika sehemu kubwa ambako serikali haifiki kwa urahisi.
Amesema kutokana na miundo mbinu mibovu ya usafiri, mafunzo ya matumizi ya simu kwa kiasi kikubwa yataongeza ujuzi katika taaluma ya upashaji habari.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 7 mwezi Februari 2014 yanalenga kutambua uwezo wa simu katika kutafuta na kutoa habari, kujifunza jinsi Tehama inavyorahisisha mawasiliao kwa njia ya simu aina ya “SMART” na kuboresha mbinu za upatikanaji na utoaji wa habari.
Mafunzo ya Tehama kwa redio jamii ni mwendelezo wa mradi wa kuzipatia uwezo redio hizo kwa kutumia teknolojia mpya unaofadhiliwa na UNESCO kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA).
DSC_0397
Mkufunzi na Mtaalamu wa Masuala ya Redio Jamii Mama Rose Haji Mwalimu kutoka UNESCO, akieleza madhumuni ya mafunzo kwa washiriki, katika Ukumbi wa Mazingira Kibaoni, Ifakara.
20140204_155711
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya TEHAMA kutumia simu kwa mawasiliano wakifanya kazi za vikundi.
20140204_155841
Washiriki katika vikundi kazi wakitumia simu zao kufanya mazoezi kutokana na mafunzo waliyopata kwa mawasiliano rahisi vijijini.
IMAG0275
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi pamoja na washiriki wa Redio Jamii kutoka Pangani, Pambazuko, Kyela, Pemba na Unguja.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU