Thursday, April 3, 2014

CHELSEA HOI KOMBE LA UEFAKombe la UEFA timu ya PSG  wakicheza Uwanja wa kwao PARC DES PRINCES huko PARIS, FRANCE, wameichapa CHELSEA Bao 3-1 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Alikuwa mchezaji Lavezzi alitangulia kuwapa PSG Bao la kuongoza katika Dakika ya 4 baada kuweka gambani Mpira uliookolewa kwa Kichwa na John Terry na kufumua Shuti moja kwa moja na kumpita Kipa PETR CECH.

CHELSEA walisawazisha kwa Penati ya Dakika ya 27 iliyopigwa na Eden Hazard na ilitolewa na Refa baada ya mchezaji OSCAR kuangushwa kwenye eneo la hatari.

PSG walifunga Bao lao la 2 baada ya mchezaji yuleyule  LAVEZZI kupiga Frikiki safi ambayo Kipa wa CHELSEA  alishindwa kuzuia na kumparaza Ibrahimovic kisha Mchezaji wa Chelsea David Luiz kuusindikiza wavuni.

Akitokea benchi mchezaji , JAVIER PASTORE, aliipa PSG Bao la 3 katika Dakika ya 90 baada ya kupokea Mpira wa kurushwa na kuwatoka Cesar a, Frank Lampard na JOHN TERRY kisha kupiga Shuti la chini chini na kumshinda Kipa wa CHELSEA

Nayo timu ya Real Madrid, wakicheza Uwanjani kwao Santiago Bernabeu Jijini Madrid Nchini HISPANIA  wameichapa BORUSSIA DORTMUND Bao 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

GARETH BALE ndie aliefunga Bao la Kwanza katika Dakika ya 3 tu baada kuunganisha pasi safi ya Daniel Carvajal na kumzidi akili Kipa Roman
Bao la Pili la Real lilifungwa katika Dakika ya 27 kupitia Isco kwa Shuti la chini toka Mita 20.

Hadi Mapumziko Bao zilikuwa Real 2 Dortmund 0.

Katika Dakika ya 57, Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, alipiga Bao la 3 baada kumtoka Kipa ROMAN kufuatia kupokea pasi safi ya Luka Modric.

Hilo ni Bao la 14 kwa Ronaldo kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu na ameifikia Rekodi  ya Lionel Messi aliefunga Bao 14 katika Mechi 11 za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 2011/12 wakati Ronaldo amechukua Mechi 8 tu.

Ronaldo hakumaliza Mechi hii baada ya kuumia na kutolewa nje katika Dakika ya 80.

Timu hizi zitarudiana huko SIGNAL IDUNA PARK, Jijini DORTMUND, GERMANY Jumanne Aprili 8.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU