Thursday, April 10, 2014

MANCHESTER UNITED NA BARCELONA OUT UEFA



Mabingwa Watetezi wa UEFA CHAMPIONZ LIGI, BAYERN MUNICH, wametinga nusu fainali  ya Mashindano hayo ya UEFA  baada ya kuichapa MANCHESTER UNITED BAO 3-1 katika Mechi ya Marudiano ya Robo Fainali.

Katika Mechi ya Kwanza huko OLD TRAFFORD Wiki iliyopita, Timu hizi zilitoka Sare ya Bao 1-1 Kwenye Mechi hii, MAN UNITED walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 57 la Patrice Evra.
BAYERN walijibu haraka na kusawazisha Dakika 2 baadae kwa Bao la MARIO MANDZUKIC na kuongeza Bao mbili kupitia THOMAS MULLER, Dakika ya 68 na ARJEN ROBBEN, Dakika ya 76. BAYERN sasa wanaungana kwenye Nusu Fainali ya UCL pamoja na CHELSEA, ATLETICO MADRID NA REAL MADRID.

Katika mchezo mwingine timu ya BARCELONA imeaga mashindano hayo baada ya kufungwa bao moja kwa bila dhidi ya ATLETICO MADRID . Bao la Dakika ya 5 la Koke limewapa ushindi Atletico Madrid wa Bao 1-0 dhidi ya Barcelona walipocheza Uwanjani kwao Estadio Vicente CalderonKatika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya Bao 1-1 HUKO NOU CAMP Wiki iliyopita.

Kwenye Mechi hii, ATLETICO walianza kwa kishindo na mbali ya kufunga Bao hilo mapema pia walipiga Posti mara 3 ndani ya Dakika 20 za kwanza.

Hii ni mara ya kwanza kwa Atletico kuingia Nusu Fainali ya Mashindano haya tangu Mwaka 1974 na ni mara ya kwanza kwa BARCELONA  kushindwa kuingia Nusu Fainali tangu 2007.

Msimu huu, Timu hizi zimekutana mara 4 na kutoka Sare.

Atletico sasa wanaungana kwenye Nusu Fainali ya UCL pamoja na CHELSEA, BAYERN MUNICH NA REAL MADRID.Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali itafanyika Ijumaa Aprili 11

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU