Sunday, April 13, 2014

MUHIDIN GURUMO AFARIKI DUNIA


Mzee Gurumo Afariki Dunia

Sunday , 13th Apr , 2014
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Dansi nchini Tanzania ambaye alitangaza kustaafu mwaka uliopita Muhidin Maalim Gurumo amefariki dunia leo April 13, 2014 saa 9 Alasiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
                      Mrehemu Mzee Muhidini Gurumo
Mwanamuziki mkongwe na Gwiji la muziki wa dansi Tanzania Maalim Muhidin Gurumo amefariki dunia leo April 13, 2014 katika hospitali ya Taifa Muhimbili saa 9 Alasiri
.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na mwanamuziki mwenzake Hussein Jumbe, pamoja na Chama Cha Muziki Tanzania.

Kwa mujibu wa makamu wa Rais wa Chama cha Muziki Tanzania anayefahamika kwa jina la Brighton, Marehemu mzee Gurumo alipelekwa hospitalini hapo jana (April 12 2014) saa 10 alifajiri mara baada ya hali yake kubalika ghafla, ambapo alilazwa katika wodi ya Kibasila kwa ajili ya matibabu.

Wakati akiendelea na matibabu, hali ilizidi kuwa mbaya na kufikia majira ya saa 8 mchana, alifariki dunia.

Taarifa kutoka kwa meneja wake zinasema kuwa Marehemu mzee Gurumo alikuwa akisumbuliwa na taizo la mapafu kujaa maji.

Mipango ya mazishi inafanywa kushirikiana na Chama cha Muziki Tanzania, ambacho kimesema kuwa mwili wa marehemu utaagwa kesho (April 14 2014) nyumbani kwake

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU