Wednesday, April 2, 2014

RAIS KIKWETE ATEMBELEA ABERDEEN, SCOTLAND, AONGEA NA KUNDI LA WABUNGE WA UINGEREZA WANACHAMA WA BRITAIN TANZANIA SOCIETY

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kundi la Wabunge  wa vyama mbalimbali vya siasa walio marafiki wa Tanzania pamoja na wanachama wa  Britain and Tanzania Society (All Party Parliamentary Group on Tanzania, and Britain Tanzania Society) katika mchapalo walioandaa kwa heshima yake katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola katika jengo la Durbur jijini London April 1, 2014.

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu kuendesha mfano wa mtambo wa kufundishia namna ya kuchimba mafuta katika visima vilivyo bahari kuu (KCA Deutag Dart Drilling Simulator and Well Enginering System) alipotembelea Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne April 1, 2014 akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi.  Nyuma yake ni  ujumbe alioongozana nao ikiwa ni pamoja na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar Mhe Nassor  Ahmed Mazrui (kulia) na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo (wa pili kulia) Wa pili kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe Peter Kallaghe, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya katika Wizara za mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Balozi Dorah Msechu
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aipata picha ya kumbukumbu na  baadhi ya Wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya Uingereza walio marafiki wa Tanzania pamoja na wanachama wa  Britain and Tanzania Society (All Party Parliamentary Group on Tanzania, and Britain Tanzania Society) katika mchapalo walioandaa kwa heshima yake katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola katika jengo la Durbur jijini London April 1, 2014.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU