Wednesday, April 9, 2014

WASHINDI 3 BORA WA SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI VYA UIGIZAJI TANZANIA LIJULIKANALO KAMA TANZANIA MOVIE TALENTS KWA KANDA YA ZIWA KUPATIKANA

Majaji wa Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents, Single Mtambalike (kulia), Yvonne Chery (Katikati) na Roy Sarungi (Kushoto) wakipitia alama za washiriki kwaajili ya kuweza kuwatangaza washindi waliofanikiwa kuingia hatua ya tatu ambapo wanachukuliwa washiriki 30 kwaajili ya kupata mchujo wa washindi watatu bora ambao wataibuka na Kitita Cha Shilingi laki 5 kila Mmoja kwa Kanda ya Ziwa na baadae kujiunga na washindi wengine watatu kutoka kila kanda katika fainali ya mwisho itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na Mshindi Kujinyakulia Zawadi Kubwa kabisa ya Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania. (50,000,000/=)
 Baadhi ya washiriki wakionyesha uwezo wao wa kuigiza mara baada ya kupewa muswada (script).
Baadhi ya washiriki wakiwa mbele ya majaji (hawapo pichani) kwaajili ya kutajwa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya tatu ambapo washiriki 30 tu ndio watachukuliwa kwaajili ya kupatikana washindi watatu watakaoibuka na kitita cha Shilingi laki 3 kila Mmoja na Baadae kuungana na washindi wengine wa kanda zilizobakia katika Fainali ya mwisho itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wawili (wa kwanza kulia na wapili) wakiwa hawaamini kama wamechaguliwa kuingia hatua ya washiriki 30 kwaajili ya mchujo wa kupata washindi watatu wa Kanda ya Ziwa, Mkoani Mwanza
 Mmoja wa washiriki aliyefanikiwa kuchaguliwa kwa hatua ya tatu (mwenye fulana nyeupe) akipongezwa na mshiriki mwenzie ambae hakupata bahati ya kuchaguliwa kwaajili ya kuendelea na hatua inayofuata.
 Washiriki wakipongezana mara baada ya kuchaguliwa kuendelea na hatua inayofuata.
Baadhi ya washiriki waliofanikiwa kuchaguliwa kwa hatua ya tatu wakishangilia mara baada ya kuchaguliwa.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU