Saturday, April 30, 2011

OLIMPIKI MAALUM WANAHITAJI MSAADA WA TIKETI KWA AJILI YA WACHEZAJI WAO

 Mkurugenzi wa OLIMPIKI MAALUM  FRANK MACHA akizungumza kuhusu safari ya wanamichezo kumi na moja kwenda nchini UGIRIKI kushiriki mashindano ya DUNIA ya riadhaa
Mkurugenzi wa OLIMPIKI MAALUM akimuonyesha mlemavu wa akili ambaye kwasasa anaendelea vizuri baada ya kushiriki michezo ambayo imemsaidia kumuweka katika hali nzuri na kufanya kazi katika ofisi hiyo ya kutunza vifaa.

Wachezaji wenye ulemavu wa akili kumi na moja wamechaguliwa kushiriki mashindano ya riadhaa ya DUNIA nchini UGIRIKI ambayo yamepangwa kufanyika JUNE mwaka huu.

Mkurugenzi wa OLIMPIKI MAAALUM FRANK MACHA amesema mpaka sasa wamepata tiketi sita tu hivyo bado tiketi tano kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo ,hivyo wanaomba kwa watu wenye uwezo wa kuwasaidia wachezaji hao wajitokeze kutoa msaada wa vifaa vya michezo nguo kwa ajili ya safari pamoja na tiketi ili kufanikisha safari ya wachezaji hao wenye ulemavu wa akili.

Amesema iwapo watashindwa kupata msaada huo watapeleka wachezaji wachache tu ,wachezaji hao mpaka sasa wanaendelea na mazoezi ya nje ya kambi kabla ya kuondoka nchini kwenda UGIRIKI kwenye mashindano hayo ya DUNIA.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU