Saturday, April 30, 2011

USAJILI KILI TAIFA CUP 2011


Timu zote 24 zilizothibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Taifa mwaka huu(Kili Taifa Cup 2011) zimewasilisha usajili wa wachezaji wao ndani ya mudauliopangwa. 


Timu hizo na vituo vyao kwenye mabano ni Mtwara, Ruvuma, Kinondonina Lindi (Lindi).Nyingine ni Mbeya, Iringa, Temeke na Rukwa (Mbeya), Dodoma, Tabora, Singida na
Kigoma (Tabora), Arusha, Kilimanjaro, Tanga na U23 (Moshi), Mwanza, Kagera, Mara
na Shinyanga (Mwanza) na Pwani, Morogoro, Ilala na Manyara (Morogoro).
 
Siku ya mwisho kuweka pingamizi kwa wachezaji ni Mei 2 wakati siku ya mwisho kwa
Kamati ya Mashindano kuthibitisha usajili ni Mei 3 mwaka huu. Timu zinatakiwa
kuwasili vituoni Mei 5 na mashindano yataanza Mei 7.
 
HAKI ZA TELEVISHENI KILI TAIFA CUP 2011
TFF ilitangaza tenda kwa vituo vya televisheni nchini kuonesha moja kwa moja
(live) mashindano ya Kili Taifa Cup. Vituo viwili vya televisheni vilijitokeza
kutaka haki ya kuonesha michuano hiyo.
 
Baadaye kituo kimoja kilijitoa kutokana na sababu za kiufundi wakati kingine
kilishindwa kufikia dau ambalo limewekwa na TFF ili kupata haki hizo. Dau la
kuonesha ‘live’ michuano hiyo ni sh. milioni 10. Hivyo hadi sasa hakuna
televisheni yenye haki ya kuonesha michuano hiyo.
 
Bado tunakaribisha vituo vyenye nia ya kuonesha mashindano hayo moja kwa moja
kwa mazungumzo. Hivyo tutatoa taarifa baadaye juu ya nini kinaendelea kabla ya
mashindano yenyewe kuanza, hasa hatua ya mtoano (knock out).
 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU