Tuesday, May 31, 2011

JUNI 4 MABONDIA KUPAMBANA

MCHAKATO wa Kuendeleza mchezo wa ngumi za Ridhaa Katika MKoa wa kimichezo wa ILALA, unatarajiwa kuingia katika hatua nyingine Juni 4kati ya klabu ya ngumi ya Amana na Matimbwa,
Mapambano hayo ya raundi nne, yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi uliopo bungoni Wilaya ya ILala ambapo mabondia wanne kutoka katika kila klabu, watachapana makonde.

Mabondia wa Amana watakaopanda siku hiyo ni IBrahimu Class Kg.64, Khalfani Othumani Kg 57, Kassimu Sambo Kg 54, na Saidi Ally Kg 48.Klabu ya Matimbwa itawakilishwa na MOhamedi Matimbwa Kg 64, MOhamedi Muhani Kg 57, Edson Joviki Kg 54 na MOhamedi Kumbilambali Kg 48
Akizungumza Dar es SAlaam leo Mratibu wa mapambano hayo ambae pia nikocha wa mchezo wa ngumi akishirikiana na Kinyogoli Foundition, RAjabu Mhamila Super D, Alisema mpango huo utaendelea mpaka wahakikishewamefanikiwa kuibua vibaji na kuviendeleza
Alisema tangu waanze mpango wa kuandaa mapambano mkohani humowamefanikiwa kurudisha hamasa ya mchezo huo mkoani humo na kuwataka wadau mbalimbali kutoa sapoti kwa mchezo huo ili upate kuendelea
ambapo Super D alitoa mfano wa vitu wanavyoviitaji ikiwemo posho za nauli kwa wachezaji vifaa vya kuwatia moyo na zawadi mbalimbali kwa mabondia

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU