Tuesday, May 31, 2011

MBEYA WAELEZA SIRI YA USHINDI


Wachezaji na viongozi wa timu ya Mkoa wa Mbeya ambao ndio mabingwa wa Kili Taifa Cup 2011 wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe na hundi ya Sh Milioni 40 Jumamosi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Mjini Arusha.Mbeya ilichukua ubingwa baa ya kuifunga Mwanza bao 1-0.


BAADA ya kutwaa ubingwa wa Kili Taifa Cup 2011 kocha wa timu ya Mkoa wa Mbeya (mapinduzi Stars) Juma Mwambusi amesema siri ya ushindi wa timu yake ni ushirikiano huku wadau mbalimbali wakisema mashindano ya mwaka huu yalikuwa ya aina yeke.

Akizugumza mjini hapa juzi wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro kwa ajili ya kuzipongeza timu zilizochukua nafasi tatu za juu, Mwambusi alisema kikosi chake kilikuwa kina ushirikiano mkubwa toka hatua ya makundi
Mwambusi alisema licha ya yeye na msaidizi wake Mbwana Makata kuwapa wachezaji mazoezi mazuri, ushirikiano kati ya wachezaji ndio siri kubwa ya ubingwa
Alisema kikosi chake toka kianze mashindano kimekuwa kikijituma na kila mchezaji akitoa nafasi kwa mwenzake hivyo kuwapa nafasi kubwa ya kunyanyua ubingwa kutoa kocha bora ambaye alipata Sh milioni 2, mfungaji bora ambaye alipata Sh milioni 2 na mchezaji bora wa mashindano Sh milioni 2.5.
"Siri kubwa ni ushirikiano wa wachezaji wakiwa uwanjani, viongozi na hata benchi la ufundi- nina amini kila kitu kinawezekana nawapongeza sana,"alisema Mwambusi
Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mwanza ambayo imeshika nafasi ya pili John Tegete, alisema timu yao kufika katika hatua ya fainali si kazi rahisi hivyo aliipongeza timu hiyo hasa ikizingatiwa haikufanya vizuri katika mashindano ya mwaka jana
Alisema matarajio yake yalikuwa kombe hilo liende mwanza lakini bahati haikuwa yao timu yao imeshika nafasi ya pili na kuondoka na kitita cha sh.milioni 20.Tegete alisema mashindano yalikuwa mazuri kwa kuwa kila timu ilionesha upinzani mkali lakini timu yao ikafika hatua ngumu ya fainali ambayo kila mtu alikuwa akiitaka
"Nashukuru sana kila kitu kina kasoro zake lakini kwa ujumla mashindano yalikuwa mazuri tofauti na watu walivyofikiria,"alisema Tegete.Naye Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Athuman Nyamlani, aliwapongeza viongozi wa chama cha Mpira wi Miguu Mkoani Arusha ARFA kwa kutoa ushikiano mkubwa katika kipindi cha mashindano.

Nyamlani alisema kuwa TFF imefurahishwa na ushirikiano huo hivyo umetoa nafasi kubwa kwa TFF kufikiria kuipeleka tena mashindano hayo mkoani hapoAidha Nyamlani alisema kwa ujumla mashindano yalikuwa na msisimko mkubwa kuanzia mwanza mpaka mwisho, tofauti na watu walivyofikiria.
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, aliipongeza TFF kwa kuendesha mashindano vizuri ambayo yalileta msisimko mkubwa katika Mkoa wa Arusha. “Mashinado yamekuwa mazuri na naishukuru TFF, waandishi wa habari na wadau wote waliofanikisha mashindano ya mwaka huu,” alisema Kavishe.
Alisema kampuni yake kama mdhamini mkuu wa mashindano haya itaongea na TFF kuangalia uwezekano wa kpeleka kila fainali mikoani ili kuupa kila mkoa fursa ya kuwa mwenyeji wa KIli Taifa Cup.

Katika Mkoa wa Arusha mashindano hayo yalianza hatua ya robo fainali baada ya timu nane, ambazo ni Arusha, Singida, Ilala, Kagera, Ruvuma, timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 23 Mwanza naMbeyakuingia hatua hiyo.

Katika mashindano hayo jumla ya kadi 17 zilitolewa ambapo kadi mbili zikiwa nyekundu na kadi 15 zikiwa za njano, wakati nyavu zilitikiswa mara 27 kuanzia hatua ya robo fainali mpaka fainali.
Mashindano hayo yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager na masuala ya habari kuratibiwa na Kampuni ya E
 
 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU