Ikiwa Tanzania inasherehekea miaka 50 ya UHURU, mbunifu  wa kiafrika Mustafa  Hassanali’s,  atazindua “UHURU” collection ambayo alivutiwa na muonekano wa bendera ya taifa  kama iliyopeperushwa Mt Kilimanjaro tarehe 9  Desember 1961 AFI Afrika Fashion Week iliyopo Johannesburg  Afrika Kusini.
“Mkusanyiko huo wa mavazi  umehusisha maliasili ya Tanzania, Ambao watu wake ni wenye  ukaurimu , nchi yenye utajiri wa maliasili za taifa na  pia ni nchi iliyojengeka na misingi   aloiweka Baba wa taifa, Mwalimu  Julius Kambarage Nyerere” alisema Mustafa Hassanali
Mkusanyiko huo wa mavazi  umepewa jina la UHURU. Na pia haupo tu   kusheherekea miaka   50 ya uhuru wa Tanzania bali uhuru huo kuonyesha  uwito, ubunifu na utamaduni.
Kwa kuwa taifa moja,  Mkusanyiko huo wa mavazi  utaonyesha Amani na utengenezaji wa  mavazi hayo yataielezea Tanzania kiundani kupitia mbunifu  wake kutoka Tanzania Mustafa Hassanali.
Safari ya Mustafa  Hassanali ya Afrika kusini imedhaminiwa na  Precision Air, Shirika la ndege lenye  ukuaji mkubwa Tanzania ambalo kwa   sasa  linafanya misafara  yake   mara 5  kwa wiki  kwa misafara ya  Johannesburg.
“Tunafarijika kuwa na   ushirika na Mustafa Hassanali,  ambae atafanya maonyesho  ya mkusanyiko wake wa mavazi kwa mara ya  nane Afrika kusini. Muungano wetu mpya unaangalia kutangaza biashara,utalii na  utamaduni uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini.  alisema  Afisa uhusiano wa Precision  air Annette Nkini.
Ikiwa ni mara ya kwanza  tena kwa Mustafa Hassanali, Atakuwa ni mbunifu pekee ambae atasherehekea miaka  50 ya uhuru wa Tanzanian nje ya Tanzania kwa kufanya ufunguzi wa  mkusanyiko wake wa Mavazi Afrika kusini.
“Maonyesho ya UHURU  collection yatakuwa ni maonyesho yangu ya pili AFI Africa Fashion Week na ya  nane kwa jamuhuri ya Afrika kusini, Itakayokuza mahusiano ya pande mbili kati ya  Tanzania  na   Afrika Kusini.” Aliongeza Hassanali
AFI Africa Fashion week  inamilikiwa na African Fashion Internationals Dr Precious Moloi,  itakayofanyika  Sandton Convention  Centre kuanzia tarehe  20-22  October. Mustafa Hassanali ndo mbunifu pekee kutoka Tanzania aliealikwa katika wiki ya  kujivunia na atafanya maonyesho yake   tarehe 22 October saa 10 jion


 
 
 
 
 
 
 


0 maoni:
Post a Comment