Sunday, January 29, 2012

SUPER D BOXING C OACH KUSAMBAZA DVD ZA MAFUNZO LEO KATIKA UWANJA WA JAMHURI WAKATI CHEKA NA KALAMA WAKIPAMBANA



KALAMA NYILAWILA FRANSIC CHEKA USO KWA USO na MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na
bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni
Januari 28 mwaka huu kuoneshana umwamba.
Cheka na Nyilawila hawajawahi kutwangana mpambano ambalo limewafanya
mashabiki kuhisi kuwa mabondia hao wanaogopana.

Akizungumza Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo Philemon
Kyando 'Don King' alisema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa
Jamhuri Morogoro nyumbani kwa Cheka.
Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 10 uzito wa kg 72

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki
kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri
Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa
na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni
mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya
utangulizi.

Alisema kutakuwa na pambano kati ya Maneno Osward [mtambo wa gongo] na
Pasco Ndomba raundi nane uziti wa kg 75, Chaulembo Palasa na Deo Njiku
kg 68, Venance Mpoji na Ibrahim Clases kg 63, Anthon Mathias na Juma
Afande kg 54 na pambano la mwisho kati ya Hassan Kidebe na Arbert
Mbena kg 54 ambapo mapambano hayo yatakuwa ya raundi sita kila moja.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU