Monday, October 25, 2010

KLABU YA STINGRAYS YA DSM YATWAA MEDALI 74 KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA YALIYOFANYIKA NCHINI MALAWI

Timu mzima ya STINGRAYS SWIM CLUB pamoja na viongozi wao
CHRISTIAN OPPERMAN amepata medali saba gold 6 na silver 1
watoto hao wakijiandaa kuogelea .

Timu ya kuongelea ya STINGRAYS ya Jijini DSM imeshika nafasi ya tatu katika mashindano ya kuongelea ya kimataifa yaliyofanyika nchini MALAWI mashindano yaliyoandaliwa na nchini ya MALAWI .

 Mmoja wa viongozi katika klabu hiyo RAMADHANI NAMKOVEKA amesema kwa mara ya kwanza klabu hiyo imeshiriki mashindano ya kimataifa na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu na kurudi nchini na medali 74 .

Mashindano hayo yalishirikisha timu mbalimbali kutoka nchini ya ZAMBIA,TANZANIA na wenyeji MALAWI.
Katika mashindano hayo ZAMBIA ndiyo walishika nafasi ya kwanza wakifuatiwa na MALAWI wenyewe pamoja na TANZANIA ambao waliwakiriswa na timu mbili kutoka ARUSHA na DSM.




0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU