Jukwaa la tatu la Swahili Fashion Week linawakutanisha pamoja wabunifu wa mavazi kutoka Afrika hasa zile nchi zinazoongea lugha ya Kiswahili, litafanya usaili kwa ajili ya kuwapa wanamitindo watakaopewa nafasi ya kuonesha mavazi ya wabunifu mbalimbali wakaoshiriki katika jukwaa hilo kubwa la mavazi AfrikaMashariki.
Usahili huo upo wazi wanawake na wanaume ambao wanapenda kuwa wanamitindo, na utafanyika katika hoteli ya Southern Sun Kuanzia saa 7 mchana.
Lengo ni kutoa nafasi kwa wale wote wenye nia ya kuwa wanamitindo kupata fursa ya kushiriki katika Swahili Fashion Week 2010.
Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.
Swahili Fashion Week 2010 imedhaminiwa na Southern Sun, home of Swahili Fashion Week, Origin Africa, USAID Compete, MALARIA HAIKUBALIKI, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania), Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print Ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danishmake up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery Ltd, 1&1 Internet Solutions, Sengi Tours, Ifashion, 361 Degrees na EATV & East Africa Radio.
0 maoni:
Post a Comment