Monday, October 25, 2010

VILABU VYA LIGI KUU KUKAGULIWA MATUMIZI YA FEDHA KATIKA AKAUNTI ZAO

Rais wa TFF LEODGER TENGA akiwa na Mkurugenzi wa Ufundi SUNDAY KAYUNI.

Shirikisho la soka nchini TFF limesema klabu ambayo itashiriki ligi kuu TANZANIA BARA hapo mwakani lazima ikaguliwe matumizi ya fedha katika akaunti ya klabu ili kuweka imani ya matumizi ya fedha katika klabu, Pamoja na vilabu kuwa na mahali pa kufanyia mazoezi maalum.

Rais wa shirikisho la soka hapa nchini LEODGER TENGA amesema mpango huu umetolewa na shirikisho la soka DUNIANI FIFA kwa lengo maalum la kuendeleza mpira pamoja ,na vilabu  viweze kuwa  na hadhi yake ukilinganisha na miaka ya nyuma

Amesema FIFA na CAF wanatarajia kutoa vitabulisho maalum kwa vilabu ili  vilabu viweze kutambuliwa , vilabu vitapata vitambulisho hivyo iwapo vitafuata  masharti hayo ambayo mojawapo ni kuwa na timu za vijana, kuwa na viwanja vya mazoezi .

Pia TENGA amesema ili ligi kuu iweze kuwa na hadhi na mwelekeo mzuri bila kuwepo na migogoro katika ligi hiyo TFF inaunda kamati  maalum ambayo itakuwa inasimamia ligi kuu TANZANIA BARA ili  jambo lolote linalotokea kuhusiana na ligi kamati hiyo itashughulikia

Amesema watakaa na vilabu vya ligi kuu kuzungumzia mipango hiyo  iwapo klabu haitatekeleza mambo hayo haitaruhusiwa kushiriki ligu TANZANIA BARA.

2 maoni:

Anonymous said...

Ni vema kufanya hivyo kwani wachezaji wengine hawana mpangilio mzuri wa fedha.
Unakuta mchezaji pesa anazopata wanatumia katika mambo yasiyo ya lazima.

Anonymous said...

Ni vema kufanya hivyo kwani wachezaji wengine hawana mpangilio mzuri wa fedha.
Unakuta mchezaji pesa anazopata wanatumia katika mambo yasiyo ya lazima.

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU