Shirikihso la ngumi za ridhaa nchini BFT limesema kuwa kipengele kinachowataka mabondia kuweka rekodi yao kama wamepimwa ukimwi kitakapowekwa na shirikisho la ngumi za ridhaa duniani AIBA kitasaidia sana kupata mabondia wenye upinzani mkubwa.
Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa BFT MAKORE MASHAGA wakati wa mahojiano maalumu na TBC ambapo amesemsa kipengele hicho kwa sasa hakipo lakini kikiwekwa kisheria kitaweza kusaidia katika kujua hali za mabondia ili kuondoa matatizo katika ulingo.
Amesema kuwa endapo watagundua kuna bondia ana taizo hilo, watampa ushauri wa namna gani ya kuendeela na mchezo huo au ikibidi kumweleza kuachana kabisa na mchezo huo .
Katika hatua nyingine, MASHAGA amevitaka vyama vya michezo huo vya mikoa kuharikisha uthibitsho wao wa mashindano ya taifa yatakayofanyika mwakani ambayo yatapata wachezaji wa timu ya taifa.
0 maoni:
Post a Comment