Baraza la michezo nchini BMT limeundwa kamati maalumu ya kuratibu michezo ya wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania,(SHIMISETA) baada ya kugundua kuwa viongozi waliokuwepo wamemaliza muda na wanaongoza shirikisho hilo kinyemela.
Afisa habari mwandamizi wa baraza la michezo (BMT) JOHN CHALUKULU amesema kwa sasa jukumu la kusimamia michezo litakuwa chini ya kamati teule na kuzitaka halmashauri kuendelea na maandalizi huku katibu mkuu wa kamati ya muda SALEH LUBANA akisema tayari wameandaa rasimu ya katiba na inatarajiwa kupitishwa na mkutano mkuu utakaofanyika kipindi cha michuano hiyo
Michuano hiyo itakayofanyika mjini MOROGORO itaanza kutimua vumbi NOVEMBA 27 na itafikia tamati yake desemba 5 mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment