wamiliki wa timu ya AFRIKA LYON
Baadhi ya wachezaji na waalimu wa AFRIKA LYON
Klabu ya AFRICAN LYON ya jijini DSM, leo imetangaza rasmi nia yao ya kutaka kubadilisha jina la klabu hiyo kufuatia klabu hiyo kubadilisha menejimenti ya klabu hiyo ili kuongeza fursa ya kuwa na wawekezaji wa klabu hiyo.
Mkurugenzi wa timu hiyo RAHIM ZAMUNDA KANGEZI ametoa kipindi cha miezi SITA kwa wadau wa eneo la TEMEKE kupendekeza jina kati aya majina MATATU ambayo ni AFRICAN LYON, TEMEKE FC na FC DSM
Naye rais wa klabu hiyo NABIL NASSOR amesema uongozi wake una mikakati mingi ikiwemo kuleta wawekezaji wengine ili kuhakikisha inainua soka hapa nchini na kukuza vipaji vipya.
0 maoni:
Post a Comment