Mchujo wa kuwatafuta wanamitindo wenye sifa za kitofauti yaan i" Giaffe unique model " utafanyika jumamosi hii ya tarehe 20 mwezi wa kumi na moja katika hoteliyenye hadhi ya nyota nne Giraffe ocean view hotel katika ukumbi wa jet 1.
Akiongea na blog zote maarufu nchini Tanzania mratibu wa shindano hilo bwanamagese Methuselah Magese amesema kuwa unique model ni shindano la kizalendo lenye nia mahususi ya kukuza tasnia ya mitindo na wanamitindo wachanga nchini Tanzania kwa kuleta umoja,mafanikio na kuhimiza mapinduzi ili tasnia hii iwe ajira kamili kwa wanamitindo wa hapa nchini kinyume na ilivyo sasa.
Magese amesema ikiwa vyombo vya habari vitaunga mkono mapinduzi haya kwa kutangaza habariza mitindo,wamamitindo na wabunifu wa ndani kwa wingi itageuza mtazamo wa watanzania wengi kuondokana na utamaduni wa kuvaa nguo za kutoka nje ya nchi pekee badala yake waqpende kuvaa nguo zilizobuniwa na wabunifu wa Tanzania.
Hii itachangia wabunifu kuwa na kipato kikubwa na maonyesho ya mavazi yatakuwa mengi ambapo wanamitindo watafaidika kwa kulipwa kwa kiwango chajuu,aidha vyombo vya habari vikitangaza sana tasnia hii jamii itapenda zaidi hata makampuni mengi yatajitokeza kuwekeza na kujitangaza kwa kudhamini shughuli za mitindo nchini Tanzania kitu ambacho kitaongeza pato la taifa na kpato cha mtu mmojammoja.
0 maoni:
Post a Comment