Tuesday, November 30, 2010

MWENYEKITI YANGA NCHUNGA AWAPIGIA MAGOTI MAKAMU DAVIS MOSHA NA LOUIS SENDEU

 LOUIS SENDEU kushoto pamoja na mwenyekiti wa YANGA NCHUNGA na Makamu mwenyekiti MOSHA wakiwa klabuni YANGA mbele ya waandishi wa habari wakitangaza kumaliza mgogoro
  NCHUNGA NA MOSHA wakati wa mkutano na waandishi wa habari
Mwenyekiti wa YANGA LLYOD NCHUNGA na Makamu mwenyekiti DAVIS MOSHA baada ya kumaliza mgogoro wao sasa mambo safi

Hatimaye Mwenyekiti wa YANGA LLYOD NCHUNGA amemaliza mvutano wa uongozi ndani ya klabu hiyo na kuwarejesha  makamu mwenyekiti wa YANGA DAVIS MOSHA pamoja na msemaji LOUIS SENDEU kuendelea na kazi ya kuitumikia yanga.

Kabla ya mwenyekiti kutoa uwamuzi huo makamu mwenyekiti DAVIS MOSHA aliwaambia waandishi wa habari kuwa licha ya kurejesha bado ataendelea na msimamo wake iwapo baadhi ya viongozi watenda kinyume na makubaliano yao

MOSHA amesema mwenyekiti hawezi kufanya kazi bila makamu mwenyekiti hivyo alishangazwa na kauli ya mwenyekiti kutangaza kuwa mambo yanayohusu klabu ya YANGA yatazungumzwa na mwenyekiti pamoja na katibu mkuu wakati msemaji yupo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa YANGA LLYOD NCHUNGA amesema  wamemaliza tofauti zao kwani mambo yaliyotokea yalikuwa ni matatizo madogo hivyo wapo pamoja kuitumikia klabu ya YANGA

Hivi karibuni uongozi wa YANGA uliwapiga marufuku makamu wa YANGA DAVIS MOSHA pamoja na msemaji LOUID SENDEU kutozungumzia masuala la YANGA kutokana na katiba ya yanga inavyosema.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU