Wednesday, December 1, 2010

NDOVU SPECIAL MALT YAZINDUA KOPO LA DHAHABU LENYE UJAZO WA 330ML.

Meneja wa bia ya ndovu OSCAR SHELUKINDO pamoja na mpishi mkuu wa TBL Bwana Gaudence Mkolwe baada ya kuzindua ndovu ya kopo

                                       Wakifurahia uzinduzu wa bia ya kopo ya ndovu

Meneja wa bia ya ndovu OSCAR SHELUKINDO pamoja na mpishi mkuu wa TBL Bwana Gaudence Mkolwe baada ya kuzindua ndovu ya kopo pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TBL
Meneja wa bia ya ndovu OSCAR SHELUKINDO pamoja na mpishi mkuu wa TBL Bwana Gaudence Mkolwe baada ya kuzindua ndovu ya kopo
Meneja wa bia ya ndovu OSCAR SHELUKINDO pamoja na mpishi mkuu wa TBL Bwana Gaudence Mkolwe baada ya kuzindua ndovu ya kopo

Dar es Salaam, Desemba 1, 2010: Kampuni ya bia nchini TBL  kupitia bia yake ya Ndovu Special Malt  imezindua kopo la dhahabu lenye ujazo wa 330ml. Kopo hili litapatikana sokoni pamoja na chupa ya kijani yenye foil ya dhahabu tunayoifahamu.

Akizungumza katika uzinduzi huo,meneja wa bia ya Ndovu Special Malt Oscar Shelukindo alisema kopo hili lenye muonekano wa kipekee unasherehekea bia ya Ndovu Special Malt kushinda tuza ya juu ya ubora ulimwenguni ijulikanayo kama Grand Gold Quality Award 2010 mwezi Mei katika  International Monde Selection. “Hii ni Grand Gold ya kwanza kutunukiwa bia nchini Tanzania na tuzo hili hutolewa kwa bia yenye ubora wa asilimia 90 hadi 100 kwa ubora unaodhibitishwa na jopo la majaji wa kimataifa” alisema Shelukindo.

Kwa upande wake mpishi mkuu wa TBL Bwana Gaudence Mkolwe alisema “Ndovu Special Malt ndiyo bia pekee iliyotengenezwa kwa Crystal Malt,ambayo inaipatia bia ya Ndovu ladha nzuri ya kipekee zaidi”.

Alisema nia na  madhumuni ya kuzinduliwa kwa bia ya Ndovu Special Malt katika  muonekano wa kopo ni kuwapa wanywaji wa bia hii nafasi ya kufurahia ubora wa Ndovu bila usumbufu wa kurudisha chupa kwa kuwa Kopo ni rahisi kubeba,Ni la kisasa na linakupa Uhuru wa kufurahia Ndovu Special Malt wakati wote.

Naye meneja wa mawasiliano na habari wa TBL Bi  Edith Mushi alisema Ndovu Special Malt inawajali wanywaji na itaendelea kuwaletea mambo mengi mazuri huku Ikitambuliwa kama bia yenye ubora zaidi nchini Tanzania.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU