Friday, November 5, 2010

TENGA HUYOO KENYA KUSULUHISHA MGOGORO WA SOKA NCHINI HUMO

Mkurugenzi wa ufundi TFF SUNDAY KAYUNI akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na ligi kuu tanzania bara,safari ya TENGA nchini KENYA pamoja na ligi daraja la kwanza
RAIS WA TFF TENGA.

RAIS wa SHIRIKISHO la soka nchini TFF, LEODGER TENGA yupo nchini KENYA kwaajili ya kufanya usuluhishi katika mgogoro wa kisoka unaohusu nani ana haki ya kuongoza soka la nchi hiyo.

TENGA, amekwenda nchini humo akiwa kama mjumbe wa kamati ya wanachama wa shirikisho la FIFA

Hivi karibuni serikali ya KENYA kupitia waziri wa michezo OTUOMA NYONGESA amesema serikali yake inakusudia kuchukua hatua za kuondoa utawala wa kisoka nchini humo kwa kuwa hairidhishwi na uendeshaji wa mchezo huo.

Aidha waziri NYONGESA alisema serikali yake haivumilii kuona Chama cha SOKA KENYA LIMITED (FKL) kinashindwa kukidhi matakwa ya uhajibikaji na uwazi, huku FIFA ikilitambua FKL tangu mwaka 2008.

Kwenda kwa TENGA nchini KENYA ni kutaka kufikia uamuzi wa usuluhisho wa kuepuka nchi ya KENYA kufungiwa na FIFA endapo serikali ya nchi hiyo itaingilia FKL.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU