JUMA KASEJA KIPA WA SIMBA (TANZANIA ONE).
Kipa wa kutegemewa wa klabu ya SIMBA kafungiwa kucheza mechi tatu za Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na utovu wa nidhamu aliounyesha wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya SIMBA na YANGA .
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF SUNDAY KAYUNI amesema KASEJA alikataa kusalimiana na mgeni rasmi wakati wa mchezo huo kitendo ambacho ni kukiuka kanunu na sheria za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kutokana na kitendo hicho mchezaji huyo amepigwa faini ya Laki Tano pamoja na kutocheza mechi tatu za ligi kuu katika hatua nyingine klabu ya yanga imepigwa faini ya Laki Tano kutoka na mashabiki wake kumfanyia fujo mshika kibendera namba mbili kwa kumtupia makopo ya maji.
0 maoni:
Post a Comment