hapa mwenyekiti wa TOC akitoa vyeti kwa waalimu wa riadha
mmoja wa wanariadha
Baadhi ya waalimu wa riadha
Walimu wa riadha baada ya kumaliza mafunzo ya wiki mbili tayari kupokea vyeti
Chama cha riadha hapa nchini na makocha wa mchezo wa riadha wameunga mkono kauli ya rais JAKAYA KIKWETE aliyoitoa bungeni mjini DODOMA hapo jana akisisitiza uwepo wa waalimu wenye sifa za kufundisha na kukuza vipaji vya wanafunzi wawapo shuleni hususani kupitia michezo mashuleni.
Katibu wa Riadha Tanzania SULEIMAN NYAMBUI ameyasema haya wakati wa kuhitimisha mafunzo ya ukocha wa riadha ngazi ya kimataifa hatua ya pili inayotambuliwa na shirikisho la riadha la kimataifa IAAF
Mafunzo ya walimu wa makocha wa riadha yamefanyika kwa lengo la kutoa maelekezo kuhusu umuhimu wa kufundisha zaidi kuhusu mchezo wa riadha ambao kwenye miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa haifanyi vizuri.
0 maoni:
Post a Comment