Tuesday, December 7, 2010

IVORY COAST NA ETHIOPIA ZATINGA NUSU FAINALI HUKU MALAWI NA ZAMBIA ZIKITOLEWA


Timu ya taifa ya IVORY COAST imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la CECAFA, TUSKER CHALENJI baada ya kuilaza MALAWI goli moja kwa bila.

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa taifa jijini DSM ulishuhudia mchezaji wa IVORY COAST KIPRE CHECHE akiipatia goli la ushindi timu yake dakika ya  themanini na moja

Mchezo uliopigwa awali timu ya taifa ya ETHIOPIA iliiilaza CHIPOLOPOLO ya ZAMBIA magoli mawili kwa moja,
Magoli ya ETHIOPIA yaliwekwa kimiani na TESTIFAYE dakika ya 18 na OMODU OKWI dakika ya 25 wakati lile la kufutia machozi kwa ZAMBIA lilifungwa na FELIX NSUNZU.

Sasa ETHIOPIA itakabiliana na IVORY COAST katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa siku ya ALHAMISI.

Hapo kesho ZANZIBAR HEROES itaingia dimbani kuumana na mabingwa watetezi UGANDA, ilhali KILIMANJARO STARS itaingia dimbani kucheza na AMAVUBI ya RWANDA katika michezo ya  robo fainali ya pili.

Kumbuka mshindi kati ya ZANZIBAR na UGANDA atacheza na mshindi kati ya KILIMANJARO STARS na RWANDA katikanusu fainali.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU