Kampuni ya simu za mkononi ya VODACOM imekabidhi hundi ya shilingi MILIONI MIA MOJA NA TISINI kwa shirikisho la vyama vya soka Afrika ya mashariki na kati CECAFA kama udhamini wake katika mashindano ya CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP yanayoendela jijini DSM.
Akizungumza wakati wa kupokea hundi hiyo rais wa CECAFA LEODGER TENGA amesema udhamini huo umekuja wakati muwafaka na utasaidia kukuza soka la ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.
Kwa upande wake Meneja udhamini wa Vodacom GEORGE RUHIMBIZA amesema VODACOM wameamua kudhamini mashindano hayo kwa kuwa wao ni washiriki halisi katika maendelao ya soka TANZANIA na hivyo wanapenda pia kufanya hivyo kwa nchi wanachama wa CECAFA.
Mashindano ya CECAFA TUSKER CHALLENGE yameingia katika hatua ya Robo fainali huku mashabiki wakilipa kiingilio cha chini cha shilingi ELFU MOJA na cha juu cha ELFU TANO baada ya kuingia bure katika michezo kadhaa ya hatua ya makundi.
0 maoni:
Post a Comment