Kocha wa timu ya KENYA JACOB MULEE akiwa na kamati ya ufundi ya timu hiyo
nahodha wa timu ya KENYA JAMES SITUMA .
TIMU ya TAIFA ya KENYA, HAREMBEE STARS imetishia kutocheza mchezo wake wa mwisho wa CECAFA TUSKER CHALENJI kutokana na kutopatiwa posho zao na shirikisho la soka la KENYA.
Wakitangaza uamuzi huo kocha wa timu hiyo JACOB MULEE na nahodha wa timu hiyo JAMES SITUMA wamesema uamuzi huo hausishi matokeo mabaya waliyoyapata katika mashindano yanayoendelea ila ni kutopatiwa fedha zao walizokubaliana.
Kocha MULEE amesema amejaribu kuongea na wachezaji wake kuachana na uamuzi huo lakini imeshindikana .
HARAMBEE STARS imepata matokeo mabaya katika mashindano ya CECAFA ya mwaka huu na mchezo wa kukamilisha ratiba utakuwa ni dhidi ya timu ya UGANDA, THE CRANES.
Naye makamu rais wa kampuni inayoshughulikia soka nchini KENYA (KFL) ERASTUS OKUL ameiambia TBC kwa njia ya simu kuwa yeye na wenzake wanalishghulikia suala hilo ambapo watahakikisha kuwa madai yao yanafanyiwa kazi na kuondokana na aibu hiyo.
Wakati huhuo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Emmanuel Nchimbi ametoa pongezi za dhati kwa Baraza la Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la ‘Challenge’ kwa mwaka 2010.
waziri CHIMBI amesema wizara yake itaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kupata burudani kwa kuwapatia wadhamini wa kuchangia gharama za uendeshaji wa michuano hiyo, hivyo kuwezesha watazamaji na wapenzi wa soka kupata unafuu wa kuingia uwanjani.
Wizara imeipongeza Kampuni ya Vodacom kwa kukubali kuchangia gharama za michezo kuanzia hatua ya Robo Fainali ili wananchi, washabiki na wapenzi wa soka waweze kuiona kwa gharama nafuu zaidi.
0 maoni:
Post a Comment