Monday, December 6, 2010

KOCHA WA ZAMBIA ASEMA TIMU YAKE ITAFIKA MBALI KATIKA MASHINDANO YA CECAFA

wachezaji wa ZAMBIA baada ya kumaliza mazoezi na kocha wao BONETTI

 
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zambia MARIO BONETI amesema ana imani kuwa timu yake itafanya vema katika mchezo wa robo fainal dhidi ya ETHIOPIA utakaopigwa katika uwanja wa taifa jijini DSM

Akiongea wakati wa mazoezi ya timu yake kocha BONETTI amesema timu zote zilizoingia hatua ya roba fainali zimejiandaa vema alakini yeye lengo lake ni kuibuka na ubingwa

Katika hatua nyingine kocha huyo amewasifu wapenzi wa soka wa TANZANIA kwa kujitokeza kwa wingi katika kila mchezo wa michuano ya kombe la TUSKER

Kwa upande wake mshambuliji wa timu hiyo FELIX NSUNZU yeye amedai ataendelea kujituma zaidi ili kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo lakini pia hakusita  kueleza mapenzi yake ya kucheza ligi ya Tanzania Bara hasa akiitaja klabu ya YANGA

Robo fainali ya kwanza ni hapo kesho ambapo ZAMBIA itacheza na ETHIOPIA huku MALAWI ikikabiliana na IVORY COAST.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU