Monday, December 6, 2010

ROBO FAINALI CECAFA TUSKER CHALLENGE KIINGILIO BUKU

Shirikisho  la soka nchini TFF limefanya kufuru baada ya kunguza viiingilio katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la CHALENGE inayoendeela jijini DSM, ambapo kiwango cha chini kitakuwa shilingi elfu moja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM,kaimu katibu mkuu wa TFF SUNDAY KAYUNI amesema kuwa uamuzi huo ni kuwawezesha mashabiki kundelea kuingia kwa wingi kufurahia michezo hiyo.

Mbali na kiiinglio cha shilingi elfu moja, pia viingilio vingine ni kati ya elfu tatu,elfu nne na viti maalumu vitakuwa ni elfu tano.

Hatua hiyo inaanza kesho ambapo hakutakuwa na dakika nyongeza katika michezo hiyo huku timu za ZAMBIA itambana na ETHIOPIA,na IVORY COAST itacheza na MALAWI hapo kesho.

Ambapo michezo mingine itafanyika jumatano kwa TANZANIA BARA kuvaana na RWANDA huku ZANZIBAR ikichuana vikali na UGANDA.

Nusu fainali ya michuano hiyo itafanyika alhamisi ambapo KAYUNI amewataka wapenzi wa soka nchini kuwa na nidhamu wanapokaaa  kwenye majukwaa.


1 maoni:

Anonymous said...

Tatizo watanzania wanapenda vya bure hata kishusha mpaka jiti 3(300) watanzania watalia tu!

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU