Monday, December 13, 2010

RAIS KIKWETE ATAKA KIKOMBE CHA CECAFA KIENDELEE KUBAKI NCHINI

                                  Rais KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE pamoja na waziri wa habari vijana utamaduni na michezo wakikabidhiwa kikombe cha CECAFA na nahodha wa KILI STARS NSAJIGWA baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa 2010
                                            Baada ya kupokea kikombe picha ya pamoja
                                         Mwakimba kulia pamoja na baadhi ya wachezaji
                               Majuto Omary akiwa na wachezaji IKULU

                             NGASA pamoja na NDITI wakiwa wametulia IKULU



Baada ya kunyakua ubingwa wa michuano ya kombe la CECAFA CHALENJI hapo jana kwa kuifunga IVORY COAST kwa bao moja kwa bila, timu ya taifa ya Tanzania Bara KILIMANJARO STARS hii leo imemkabidhi rasmi kombe kwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.

Kikosi hicho cha Kili Stars kiliwasili IKULU majira ya saa saba kamili za mchana huku kila mchezaji akionesha nyuso ya furaha kuashiria kumaliza kiu ya ubingwa iliyodumu kwa takribani miaka kumi na sita.

Nahodha wa Kili Stars SHADRACK NSAJIGWA ndiye alikuwa na jukumu la kumpatia kombe hilo rais KIKWETE sambamba na mkewe MAMA SALMA ambao  kwa mapenzi makubwa walibusu kombe hilo kama ishara ya upendo na furaha ya ushindi.

Baada ya kupokea kombe hilo rais KIKWETE alitoa pongezi kwa vijana wa KILI STARS na hasa akilipongeza shirikisho la soka nchini (TFF) kwa uongozi thabiti unaojali maendeleo ya soka

Rais pia alitoa angalizo kwa timu hiyo kutoridhika na ushindi huo na kuitaka ihakikishe kuwa kombe hilo linabaki nchini mwaka ujao na pia iweke mikakati madhubuti ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2014

Katika hafla hiyo pia chama cha waandishi wa habari za michezo nchini (TASWA) kilitoa tuzo maalumu kwa rais kama ishara ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya michezo na sanaa nchini tangu aingie madarakani mwaka 2005.

KILIMANAJARO STARS imebidi isubiri kwa miaka 16 kabla ya hiyo jana kufuta ukame wa muda mrefu wa kuibuka na kikombe, kwa mara ya mwisho KILIMANJARO STARS ilinyakua kombe hilo mwaka 1994.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU