Monday, December 13, 2010

WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO WALIPOGOMA IKULU BAADA YA BAADHI YA WAANDISHI KUTOLEWA NJE

                                 Mbele SAID KILUMANGA na baadhi ya waandishi walipogoma
                                   Waandishi wa michezo wakipanga mikakati ya kuendeleza mgomo IKULU
                              Majuto Omary amemshika bega Mwenyekiti wa TASWA JUMA PINTO IKULU Jijini DSM
Makamu mwenyekiti wa TASWA KITENGE akijaribu kutoa ufafanuzi wa baadhi ya waandishi kutolewa nje wakati Rais KIKWETE aliwaalika wachezaji wa KILIMANJARO STARS kupata chakula pamoja na kumkabidhi kikombe
                                      Mama ASHA SAID K akiwa ndani ya mgomo IKULU Jijini DSM .

Waandishi wa habari za michezo waligoma kuendelea na kazi IKULU Jijini DSM baada ya ukumbi uliokuwa umeandaliwa kuwa mdogo hivyo kupelekea baadhi ya waandishi kutolewa nje na maafisa wa IKULU na kuwataka wabaki wapiga picha tu bila waandishi amabao ndiyo watendaji wakuu

Waandishi wa habari walilamika kuwa maneno yaliyotolewa na mmoja wa maafisa ndani ya IKULU hayakuwa siyo mazuri kwani wao walienda kufanya kazi kama walivyotakiwa kufika kwa Rais KIKWETE alipokuwa anaipongeza timu ya KILI STARS pamoja na kupokea kikombe cha CECAFA.

Lakini baada ya muda viongozi wa TASWA walifanya kazi yao na kuhakikisha kila mwandishi anapata haki ya kukaa ndani na kuendelea kazi kama kawaida

1 maoni:

Anonymous said...

Hakuna chochote, kama ukumbi ulikuwa mdogo ni rahisi to understand, mgomo gani huo, hao waandishi walikuwa wanataka wali tu hakuna chochote!

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU