Katibu mkuu wa yanga MWALUSAKO pamoja na msemaji wa klabu hiyo SENDEU wakishangaa uwanja wa ndege baada ya mdhamini wao YUSUPH MANJI kuondoka bila kuonana nao kutokana na viongozi hao kuchelewa kufiki uwanja wa ndege.
SENDEU ambaye aliwaita waandishi wa habari kufiki uwanja wa ndege kwa madai kuwa MANJA anakutana na viongozi kwa ajili ya mazungumzo lakini hali ikabadilika baada ya viongozi hao kuchelewa .
Awali MANJI aliwata viongozi wa YANGA kukutana naye uwanja wa ndege asubuhi saa moja na nusu lakini bahati mbaya viongozi wa yanga baadhi yao hawakufika na waliofika walichelewa hivyo kuwalazimu kuwaomba radhi wandishi wa habari walioitwa kwa ajili ya kushuhudia maongezi hayo,lakini pia viongozi ambao ndiyo wahusika wenyewe mwenyekiti NCHUNGA pamoja na makamu wake MOSHA hawakufika uwanja wa ndege hivyo katibu na msemaji ndiyo waliofika bila mafanikio
2 maoni:
Yanga haistahili unyanywasaji na huyu Manji; Inaweza kujitegemea kama wakijenga Uwanja Wao Wa Kaunda na Kumiliki Uuzaji wa Jezi; Hii inaonyesha Manji anavyoatumikiza viongozi wa Yanga kama Watumwa... waafrika bwana!!!!
Njaa mbaya , usikute hata kumuamkia Manji wanamuamkia ingawa kiumri mdogo.hakuna kitu kibaya kama mtu kujidhalilisha mwenyewe, ukijidhalilisha na watu watakudhalilisha daima . big up kwa Mosha na Nchunga kutoitikia wito wa Manji.
Post a Comment