Msemaji wa SIMBA NDIMBO
Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara klabu ya Simba imelitaka shirikisho la soka nchini kuangalia uwezekano wa kuondoa nyota wake katika kikosi cha timu ya taifa ili klabu hiyo iendelee na maandalizi yake ya michuano ya kimataifa
Afisa habari wa klabu ya SIMBA CLIFORD NDIMBO amesema ingawa wamewaruhusu wachezaji hao kujiunga na timu ya taifa kwa sasa wanafanya mazungumzo na uongozi wa TFF ili nafasi za wachezaji hao zichukuliwe na wachezaji wengine
Kwa sasa timu ya SIMBA imeelekea visiwani ZAZNIBAR kwa ajili ya maandalizi ya michuao ya kombe la MAPINDUZI pamnoja na ligi ya mabingwa barani AFRIKA
Katika michezo ya ligi ya mabingwa SIMBA imepangwa na ELAN CLUB DE MITSOIDJE ya COMORO na endapo itavuka hatua hiyo ya kwanza basi itakutana na mabingwa watetezi wa kombe hilo TP MAZEMBE ya JAMHURI ya KIDEMOKRASIA ya KONGO
0 maoni:
Post a Comment