shirikisho la mpira wa kikapu nchini (TBF) limeridhika na maendeleo ya mchezo huyo kwa mwaka 2010, hatua inayoonesha kuwepo kwa matumaini ya kutoa wachezaji wengi zaidi wa mpira wa kikapu kwa mwaka 2011.
Mwenyekiti wa BFT, PHARES MAGESA amesema mashindano mbalimbali ya mchezo huo pamoja na Clinic za mafunzo zilizoendeshwa na wakufunzi wa kimataifa kwa vijana vimesaidia kuinua hamasa katika mchezo wa mpira wa kikapu nchini
Aidha Magesa amesema BFT, imeandaa mpango kabambe wa kutafuta vijana wenye vipaji vya mchezo huo ili hatimaye kupata timu bora ya taifa ya mchezo wa kikapu.
katika hatua nyingine MAGESA ametoa wito kwa rais wa JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA, JAKAYA KIKWETE kuwapatia mwalimu wa kimataifa wa mchezo wa kikapu kama alivyofanya kwa michezo mingine ikiwemo soka, ngumi na mpira wa pete.
0 maoni:
Post a Comment