Mchezaji wa YANGA ALLY MSIGWA mwenye jezi ya kijani.
KAMATI ndogo ya sheria , katiba , maadili na hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka Tanzania ( TFF) imeiamuru klabu ya YANGA kumlipa fidia mchezaji wake ALI MSINGWA ambao YANGA ilikiuka mkataba na mchezaji huyo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, ALEX MGONGOLWA, amesema pande mbili zilikutana na mchezaji ALI MSIGWA alitoa sharti la kutaka kutambuliwa kama mchezaji wa YANGA au kulipwa fidia
Mwaka 2008 klabu ya YANGA ilimsajili mchezaji hadi mwaka 2013 , makubaliano ambayo kamati hiyo imeiona kuwa haikumtendea haki mchezaji huyo.
YANGA haitaruhusiwa kusajili wachezaji wengine hapo mwakani hadi ihakikishe inalipa deni la mchezaji huyo shilingi milioni SABA .
0 maoni:
Post a Comment