MSEMAJI WA YANGA LOUIS SENDEU
Klabu ya YANGA inatarajia kutumia kiasi cha bilioni 4 .5 kwa ajili ya ujenzi wa uwaja wa KAUNDA na matengezo ya jengo la klabu hiyo lililoko mtaa wa MAFIA jijini DSM.
Afisa habari wa YANGA LUIS SENDEU amesema tayari kamati ya kuendeleza miradi ya klabu hiyo iliyo chini ya MBARAKA IGANGULA imeanza utaratibu wa kuhakisha ujenzo huo unaanza mwezi JANUARI mwakani .
Aidha SENDEU amesema baada ya kumamilika uwanja huo wa KAUNDA utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki elfu ishirini na tano na utatuimia na klabi hiyo katika michezo yake mbalimbali ya ligi kuu Tanzania bara.
Wakati huohuo mchezo kati ya YANGA na JKT RUVU uliopangwa kuchezwa leo katika uwanja wa UHURU umesogezwa mbele hadi siku ya jumamosi kupisha maandalizi ya sherehe za kitaifa za mwaka mpya
Katika hatua nyingine YANGA bado inaendelea kufanya mazungumzo na klabu ya Dong Long Tan ya nchini VIETNAM iliyotenga kiasi cha dola elfu 35 kumsajili kiungo huyo wa jangwani huku klabu ya YANGA ikitaka dau la sola elfu 40 ili kumwachia nahodha wao huyo
1 maoni:
Jamani chukueni hiyo dola 35,000 si haba msajili wengine. Acheni tamaa.
Post a Comment