Saturday, January 22, 2011

MWENYEKITI YANGA NCHUNGA ASEMA HATOKI YANGA

SAKATA la kutoelewana kati ya baadhi ya wanachama wa klabu ya YANGA na mwenyekiti wa klabu hiyo , LLOYD NCHUNGA limeingia katika sura mpya baada mwenyekiti huyo kuzungumza na waandishi wa habari na kutamka kuwa katu hatojiuzulu kama wanachama hao wanavyotaka.

NCHUNGA anasema mkutano wa matawi uliofanyika jana haukuwa halali na ulikuwa ni kivuli tu  wenyeviti wa matawi ya YANGA na amelaani kitendo cha mkutano huo kuagiza kamati ya utendaji kumsimamisha.

Ndani ya klabu ya YANGA kumekuwepo na hali ya sintofahamu katika klabu ya yanga ambapo hapo jana wanachama wa YANGA kupitia matawi ya klabu hiyo walifanya mkutano wa dharura makuo makuu ya klabu hiyo na kuamua kwa kauli moja kuwa kamati ya utendaji ya klabu hiyo inatakiwa kumsimamisha mwwenyekiti wao LYOD NCHUNGA na pia waliamua kumkataa mfadhili wao YUSSUPH MANJI kwa madai kuwa fedha zake ndizo zinzoivuruga klabu hiyo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU