Saturday, January 22, 2011

PAUL LUVINGA ATWAA TUZO YA SHUJAA WA SAFARI LAGER


                                    Mshindi wa SHUJAA wa SAFARI LAGER baada ya kupokea tuzo yake
                                  Mmoja wa washiriki akikabidhiwa hundi ya milioni moja kwa kuingia fainali
                                Washiriki watatu waliokuwa wanawania nafasi ya shujaa wa safari lager
                                            Bendi ya MJOMBA ikitumbuiza
                              Mkurugenzi wa masoko wa TBL DAVID MINJA wakati wa kutangaza mshindi wa SHUJAA wa SAFARI LAGER.

Majaji wa shindano la SHUJAA wamemchagua PAUL LUVINGA kuwa shujaa wa tuzo hiyo ambaye ameshinda baada ya kuanzisha MAKTABA ya bure ya mtaani na kusaidia zaidi ya wanafunzi 200.

PAUL ambaye amejishindia kitita cha shilingi MILIONI SABA amewashinda washiriki wengine wawili ambao ni MERCY SHAYO na LEONARD MTEPA ambao wamepata shilingi MILIONI MOJA kila mmoja.

Naibu waziri wa kazi na ajira DOKTA MAKONGORO MAHANGA amesema wakati akitoa zawadi kwa mshindi huyo kuwa shindano hilo ni moja ya ukuzaji wa ajira hapa nchini.

Mshindi PAUL mbali na kujinyakulia shilingi milioni saba pia kampuni ya bia ya TBL imempa kiasi cha shilingi MILIONI TATU ili aweze kuboresha wazo lake katika kusaidia jamii inayomzunguka.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU