Saturday, January 22, 2011

YANGA YATUMA SALAM KWA TIMU PINZANI BAADA YA KUICHAPA AFC ARUSHA MAGOLI 6 KWA 1

                               
Katika  uwanja wa UHURU hapa jijini DSM wenyeji YANGA waliwaalika watoto wa ATOWN-AFC na kuwapa kipigo cha paka mwizi cha magoli SITA kwa MOJA.

Magoli ya YANGA yamepachikwa wavuni na DAVIES MWAPE aliyepachika magoli MATATU ,IDD MBAGA aliyefunga mawili na SHADRACK NSAJIGWA aliyefunga bao moja.

Huko katika uwanja wa MANUNGU COMPEX,TURIANI mkoani MOROGORO wenyeji MTIBWA SUGAR wameilaza POLISI TANZANIA goli MOJA kwa bila likifungwa na JAFFAR JUMA JAFFAR.

kwa matokeo hayo YANGA sasa wanongoza ligi wakiwa na alama 27 wakifuatiwa na mahasimu wao wa jadi SIMBA wenye alama 25 huku mtibwa wakiwa katika nafasi ya TATU na alama zao 22.


 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU