Friday, January 28, 2011

PAPIC ATOA SIKU MBILI KWA YANGA KUKAA PAMOJA KABLA YA KUONDOKA

                                           Kocha wa yanga PAPIC aliyeachia ngazi
                                Aliyekuwa meneja wa yanga MPANGALA akiwa katika pozi.

WAKATI kocha mkuu wa Yanga KOSTADIN PAPIC akipanga kuondoka nchini JUMATATU ijayo kwenda nchini mwao SERBIA, kocha huyo ametoa msimamo kwa viongozi wa YANGA kuwa ili aweze kuendelea na timu hiyo apewe nafasi ya kuchagua kocha msaidizi mwingine na si vinginevyo. 

 PAPIC, katika mahojiano yetu amekiri kuwa kwanza  anaipenda Yanga , ila uongozi wa klabu hiyo haukutenda haki pale ilipomleta kocha msaidizi ambaye FRED FELIX MINZIRO bila ya kumshirikisha kocha huyo kitu ambacho amekitaja ni ukiukwaji wa ueledi wa ukocha.

Lakini PAPIC anamalizia sakata hili kwa kusema kuwa yupo tayari kufanya kazi na viongozi wa YANGA kwa sharti la kuketi naye tena siku za Jumamosi na Jumapili.

Mbali na menejimenti yenyewe kwa yenyewe kuwa na misimamo tofauti , klabu ya YANGA ipo katika mgogoro mzito unaotokana na makundi yaliyojigawa ndani kwa ndani kitu ambacho huenda kikatoa mwanya.

1 maoni:

Anonymous said...

Dada jane naomba uniandikie mail yako nataka kuwasiliana na wew kuhusu Yanga yangaafrika@gmail.com.

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU