Wednesday, January 19, 2011

STARS YALAMBA MILIONI 75

WAANDAAJI wa michuano ya soka kwa Nchi za Bonde la Mto Nile wameipa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' sh.milioni 75, ingawa ilivurunda.

Taifa Stars ilishika nafasi ya sita kati ya timu saba zilizoshiriki mashindano hayo ya kwanza ambayo yameandaliwa na Misri,huku Burundi ikiwa ndiyo ya mwisho na Sudani imeshika nafasi ya tano, baada ya Jumapili kuifunga Taifa Stars mabao 2-0 katikamechi ya kuwania nafasi ya tano.Lakini juzi Taifa Stars, Sudani na Burundi timu vibonde katika mashindano hayo zilitangazwa kila moja kupewa dola za Marekani50,000 sawa na sh. milioni 75 za Tanzania. Mashindano yaliandaliwa na Chama cha Soka cha Misri (EFA).

Fedha hizo ziliztangazwa baada ya mchezo wa fainali ya michuano hiyo Uwanja wa Jeshi mjini hapa ambapo Misri iliibuka naushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uganda na kuibuka bingwa.

Kwa kutwaa ubingwa huo ambao unaifanya Misri kuwa bingwa wa kwanza ilizawadiwa dola 150,000 za Marekani sawa na sh. milioni225 za Tanzania, wakati Uganda iliyoshika nafasi ya pili ilizawadiwa dola za Marekani 120,000 sawa na sh.milioni 180 zaTanzania.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambayo juzi iliifunga Kenya baop 1-0 ma kushika nafasi ya tatu, yenyewe ililamba dolaza Marekani 100,000 sawa na sh. milioni 150 za Tanzania, huku Kenya yenyewe ikitia kibindoni dola 60,000 sawa na sh.milioni90 za Tanzania.

Dola moja ya Marekani kwa sasa ni kati ya sh.1460 hadi 1500 hivyo kuifanya angalau Taifa Stars nayo kupoza machungu ya kukosazawadi kubwa za mshindi wa kwanza hadi wa tatu.

Taifa Stars ambayo haikushinda mechi katika mechi ilitarajiwa kuondoka jana usiku na kufika Dar es Salaam leo alfajiri ikiwa,ikiwa imefungwa mechi mbili na kutoka sare mbili Ilifungwa na Misri mabao 5-1, ilifungwa na Sudani mabao 2-0 na ilitoka sare ya bao 1-1 na Uganda na sare kama hiyo na timuiliyoshika nafasi ya mwisho Burundi, ambayo ilipata pointi moja tu ya Stars.

Wakati huohuo, kipa Kidiaba wa DRC alitangazwa kuwa Kipa Bora wa Mashindano, huku mshambuliaji Said Khamdi wa Misri ambayemechi ya fainali alifunga mabao mawili alitangazwa kuwa Mfungaji Bora baada ya kufunga mabao sita na Ahned Said Faraj pia waMisri aliibuka Mchez
aji Bora.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU