Tuesday, January 4, 2011

TAIFA STARS KUSHUKA DIMBANI NA MISRI KATIKA KUWANIA KOMBE LA NILE BASIN

                               Rais wa TFF TENGA akiwa na Mkurugenzi wa ufundi SUNDAY KAYUNI wakati STARS akifanya mazoezi ya mwisho
                                         KASEJA akijiandaa kufanya mazoezi
                   Rais wa TFF LEODGER TENGA ikiwaasa wachezaji kabla ya kuondoka kwenda MISRI
                                   Hapa wachezaji wakiwa wamepunzika wakati baada ya mazoezi
KASEJA ,KADO makipa wa TAIFA STARS waliokwenda MISRI wakati wa mazoezi ya mwisho

TIMU ya TAIFA STARS kesho inaanza kibarua chake cha kutafuta nafasi ya kunyakuwa kwa mara ya kwanza kombe la NILE BASIN kwa kucheza na timu ya taifa ya MISRI katika mchezo wa ufunguzi huku mshambuliaji wa timu hiyo MOHAMED ABDALLAH MACHUPA na kiungo RASHIDI GUMBO wakiopangiwa kuungana na wenzao kesho.

Kaimu katibu mkuu wa TFF SUNDUY KAYUNI amewaambia waandishi wa habari jijini DSM hii leo kwamba wachezaji hao pamoja na daktari wa timu JUMA MWANKEMWA walichelewa kuondoka nchini kutokana na matatizo ya mawasiliano kati ya TFF na chama cha soka cha MISRI

KAYUNI amesema kocha mkuu wa TAIFA STARS, JAN POULSEN aliyekuwa kwao DENMARCK kwa mapunziko mafupi tayari ameshawasili MISRI kuungana na TAIFA STARS na ataiongoza katika mashindano hayo.

Mashindano ya NILE BASIN ni mahususi kwaajili ya kutunza vyanzo vya maji ya mto NILE na ndo maana nchi za KENYA, UGANDA, TANZANIA, SUDAN na wenyeji MISRI zinashiriki katika mashindano hayo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU