Monday, January 10, 2011

vIJANA 30 WACHAGULIWA KATIKA TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 20

Hapa waandishi wa habari wa TBC wakitoka katika ofisi za TFF baada ya kuongea na kocha CHARLES MKWASA .

Wachezaji 30, wamechaguliwa baadaya kumalizika kwa mashindano ya vijana ya klabu zinazoshiriki ligi kuu soka Tanzanuia Bara.

Mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya mashindano hayo CHARLES BONIFACE MKWASA amesema ana matarajio makubwa ya kupata timu bora ya taifa katika miaka ijayo kutokana na uteuzi makini uliofanywa na kamati yake.

 MKWASA amesema wachezaji hao wataitwa katika kambi ya mazoezi na kuchujwa ambapo watabaki wachezaji wachache watakaoungana na wachezaji wa timu ya taifa chini ya vijana waliovuka umri wa miaka 17 kutengeneza timu ya taifa chini ya umri wa miaka 20, NGORONGORO HEROES.

Wakati huo huo Timu ya vijana ya AFC ya ARUSHA imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michunao ya kombe la vijana wa chini ya umri wa miaka 20 inayoendelea katika uwanja wa KARUME baada ya kuifunga POLISI DODOMA mabao MAWILI kwa BILA.

AFC ya ARUSHA ilipata bao lake la kwanza katika dakika ya 28 kupitia kwa JOSEPH MSAFIRI .

Dakika mbili tu baada ya kipindi cha  pili AFC ya ARUSHA ilifanikiwa kupata bao la pili na la  ushindi lililofungwa na ZAKAYO JOSEPH.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU