Thursday, January 13, 2011

ZESCO YATUA NCHINI KUCHEZA NA SIMBA NA YANGA UWANJA W A UHURU

Timu ya ZESCO kutoka ZAMBIA imewasili nchini kwa ajili ya michezo ya kirafiki ya kimataifa na klabu za SIMBA na YANGA michezo itakayofanyika uwanja wa UHURU siku ya jumamosi na jumapili
Mwenyekiti wa chama soka mkoa wa DSM, (DRFA) AMIN BAKHRESA amesema tayari mipango ya mchezo huo imekamilika na wamefanya mawasiliano na shirikisho la soka nchini ambalo awali lilitangaza kutoruhusu michezo ya kirafiki baada ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu
ZESCO inayoongoza ligi ya ZAMBIA maarufu ‘SUPER LEAGUE’ itakabiliana na mabingwa wa ligi kuu na kombe la mapinguzi SIMBA siku ya jumamosi hii kabla ya kuivaa YANGA siku ya jumapili michezo yote ikipigwa katika uwanja wa UHURU jijini DSM.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU