Mshambuliaji wa kimataifa wa TANZANIA anayecheza soka la kulipwa nchini SWEDEN, THOMAS ULIMWENGU ametoa rai kwa wachezaji chipukizi kuongeza juhudi ili hatimaye kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
ULIMWENGU ambaye ametokea kituo cha soka cha shirikisho la soka nchini (TSA) amesema katika muda wa miezi sita aliyocheza soka la kulipwa amegundua siri kubwa ya kufanikiwa ni kujituma na kuzingatia maadaili ya soka.
THOMAS anayechezea klabu ya Athletic FC, ameongeza kuwa kwa sasa anajituma zaidi ili ang’are katika ligi ya SWEDEN hatimaye afanikiwe kuendeleza ndoto yake ya kucheza soka la kulipwa nchini UFARANSA.
THOMAS ULIMWENGU yuko nchini kwa mapumziko baada ya kuiwakilisha nchi akiwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars na kunyakua ubingwa wa kombe hilo.
miongoni mwa wachezaji wa kitanzania wanaosakata soka la kulipwa nchini SWEDEN ni pamoja na ATHUMAN MACHUPA, CREDO MWAIPOPO.
0 maoni:
Post a Comment